Ushoga ni neno pana ambalo mara nyingi linazungumzwa juu juu. Hapa nitakusaidia kupanua uelewa wako kuhusu ushoga ili kukusaidia na kukufanya uweze kuwasaidia watu uwapendao.
Kwa lugha ya kiingereza kuna maneno ambayo yamewekwa kwa mfumo wa kifupi kusomeka LGBTQ ambayo kwa ujumla wake tunatafsiri kama ushoga. Sasa tuangalie neno LGBTQ linamaanisha nini kwa kuchambua herufi moja moja.
Herufi L Inamaanisha LESBIANS maana yake ni wanawake wenye mvuto wa kingono kwa wanawake wenzao. Wengi tunawajua kama wasagaji. Wanavutiwa kukumbatiana, kupigana mabusu, kutomasana hadi kufanya ngono na wanawake wenzao.
Herufi G Inamaanisha GAYS maana yake ni wanaume wenye mvuto wa kingono kwa wanaume wenzao. Hawa ndio mara nyingi tunawaita mashoga. Kwenye hili kundi, kuna wale ambao wanawaingilia wanaume wenzao na kuna wale ambao wanapenda kuingiliwa na wanaume wenzao.
Herufi B Inamaanisha BISEXUAL maana yake ni wale ambao wanavutiwa na watu wa jinsia zote kingono. Kama ni mwanaume anaweza kuvutiwa kingono na mwanamke halafu pia anavutiwa kingono na mwanaume mwenzake. Anaweza kuwa na mpenzi, anaweza kuwa ameoa mke mzuri lakini anachepuka na rafiki yake wa kiume. Vivyo hivyo kwa wanawake. Ni mwanamke ambaye anavutiwa kingono na wanaume pamoja na wanawake wenzako pia. Anaweza kuwa ameolewa na mume mzuri lakini anamuaga mumewe kwenda kwa shoga yake kumbe ni mpenzi wake na wanafanya ngono kabisa.
Herufi T Inamaanisha TRANSGENDER maana yake ni wale ambao wana muonekano ambao unawatambulisha kuwa wa jinsia fulani tofauti na jinsia yao halisi waliozaliwa nayo. Kama ni mtu mwenye jinsia ya kiume ataonekana na mwonekano wa kimwanamke kwa nje lakini kumbe ni mwanaume. Kama ni mtu mwenye jinsia ya kike ataonekana na mwonekano wa kimwanaume kwa nje kumbe ni mwanamke. Hawa ndio tunawaita tom-boys au jike dume.
Herufi Q Inamaanisha QUEER/QUESTIONING ambao ni wale watu hawajui jinsia yao ni ipi. Wana Maumbile waliyozaliwa nayo ya kike au ya kiume lakini hawajitambulishi kama wa kiume au kama wa kike kulingana na jinsia zao.
Sasa natambua kuwa umekuja kwenye makala hii kwa lengo zuri la kumsaidia ndugu au rafiki yako kutoka kwenye ushoga. Kujua yeye ni shoga wa aina gani itakusaidia kumsaidia kimahususi. Hata hivyo, wapo wale ambao wamekuja kwenye makala kwa sababu wao ndio husumbuliwa na ushoga. Wengine wanataka kutoka huko; na wengine hawajafanya maamuzi hayo bado.
Wote mtahudumiwa na kutoka na mtazamo sahihi. Kwanza mtazamo wako ndio tunashughulika nao maana vita kubwa ipo kwenye ufahamu wako. Kuna kitu unajua ambacho sio sahihi wala sio kweli, na kuna kitu hujui.
Nitakusaidia kupitia kujibu maswali makubwa mawili: 1.Wewe ni mvulana/mwanaume na unavutiwa kingono na wavulana/wanaume wenzako? Wewe ni msichana/mwanamke na unavutiwa kingono na wasichana/wanawake wenzako?
Ulishawahi kufuatwa na mvulana mwenzako akaanza kukuonyesha vitendo vinavyoashiria anavutiwa na wewe kingono? Ulishawahi kufuatwa na msichana mwenzako akaanza kukuonyesha vitendo vinavyoashiria anavutiwa na wewe kingono?
Unashawishika kuwa na mchumba wa jinsia moja na yako?
Tuangalie biblia inatufundisha nini kuhusu kuvutiwa kingono na mtu wa jinsia moja na wewe.
Adamu alivutiwa kihisia na mtu wa jinsi yake na siyo mtu wa jinsia yake. Huyu mtu wa jinsi yake alifanywa na Mungu kuwa mwanamke, yaani “Womb-man (mtu mwenye mji wa mmba)” kwa kusudi la kuendelea uzao wa watu duniani.
Mungu aliweka mipaka ya ngono kuwa ni baina ya mwanaume na mwanamke wa jinsi inayofanana (binadamu kwa binadamu, wanyama kwa wanyama).
Kutaka kujaribu vinginevyo ni kuvuka mipaka ambayo imewekwa na Mungu mwenyewe. Na kufanya hivyo ni dhambi.
1Wakorintho 11:11 SUV
“Walakini si mwanamke pasipo mwanamume, wala mwanamume pasipo mwanamke, katika Bwana.”
Ngono haipaswi kufanywa na mwanaume pasipo na mwanamke, wala kufanywa na mwanamke pasipo mwanaume. Maana imekuzudiwa kuleta uzoa – yaani maongezeko ya watu. Ngono baina ya mwanamke na mwanamke hawawezi kuleta uzao wala ngono baina ya mwanaume na mwanaume haiwezi kuleta uzao.
Biblia inaitambulisha mipaka hii kwamba, ni katika Bwana. Nje ya hapo ni nje ya Bwana.
Swali la pili. JE UNAHISI MSUKUMO WA KUBADILI JINSIA?
Unaona hisia zako haziendani na jinsia yako, na hiyo unataka kubadilisha jinsia yako?
Neno la Mungu linasema nini kuhusu jinsia?
Mathayo 19:4 SUV
“Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,”
Yesu anawajibu Mafarisayo kwa kuwakumbusha uumbaji. Na wewe unakumbushwa, “Haukusoma Mwanzo 1:27?”
Kwamba, “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.”
Kwamba, hivi alivyoumba, mwanamume na mwanamke ndio kwa mfano wake. Halafu kuonyesha kwamba hakukosea, anafanya tathimini na kuona alichokifanya kuwa ni chema sana “very good”. (Mwanzo 1:31)
Inakuwaje wewe unaona vile Mungu alivyokuumba na hiyo jinsia yako kwamba alikosea? Kwamba ni mbaya? Unamaanisha kile Mungu anachokiona chema sana wewe unakiona kibaya?
Hata hivyo, yeye (Mungu) ndiye aliyekuumba. Maana yake ni kwamba yeye ndiye MUUMBAJI. Kazi ya kuumba ni yake, sio yako. Usijifanye mvumbuzi.
Nimeandika kitabu kwa ajili ya kuwasaidia watu kutoka kwenye ushoga. Ni kitabu kwa ajili ya vijana kuanzia miaka 13 pamoja na watu wazima. Kinaitwa I AM BORN STRAIGHT (NIMEZALIWA MKAMILIFU) ni kitabu kimeandikwa kwa lugha ya Kiswahili pamoja na lugha ya Kiingereza. Ikiwa unahitaji kupata nakala yako, wasiliana na mwandishi kwa namba za simu 0657342567.
Nakutakia matokeo chanya.
Leave a comment