Devotionals & EncouragementSwahili Articles

Nguvu ya Ukiri Sahihi

Share
Nguvu ya Ukiri Sahihi
Share

Andiko:
Ufunuo 12:11Nao wakamshinda kwa damu ya Mwanakondoo na kwa neno (logos) la ushuhuda wao…

Tafakari:
Katika maandiko ya asili, neno lililotumika hapa ni logos la Kiyunani, ambalo halimaanishi tu “neno lililosemwa,” bali pia linaonyesha kanuni ya kimungu iliyo wazi na thabiti. Kwa maneno mengine, ushindi wa waamini haukutokana na maneno ya kawaida, bali ni ukiri wenye msingi katika kanuni za Mungu.

Aidha, Mithali 18:21 inasema: “Mauti na uzima hu katika uwezo wa ulimi.” Katika Kiebrania, neno “ulimì” limetokana na neno lashon ambalo si tu kiungo cha mwili, bali ni ishara ya mamlaka ya kuamua hatima kwa kusema. Hivyo, kila ukiri wa mtu unaweza kuwa mbegu ya uhai au hukumu ya mauti.

Yesu mwenyewe alipojaribiwa jangwani (Mathayo 4:4), alitumia neno gegraptai – “Imeandikwa.” Hapa si kutaja tu andiko, bali ni kulisema kama tangazo la mamlaka. Kimsingi alisema: “Neno hili limekwisha kuamuliwa na halibadiliki.”

Hii inatufundisha kwamba ukiri sahihi si mawazo yetu binafsi, bali ni kurudia kile Mungu amesema tayari. Tunapolingana na Neno lake, ukiri wetu unakuwa ni silaha ya kiroho na tangazo la ushindi.

Nugget ya Dhahabu:
“Ukiri sahihi si maneno ya kawaida; ni logos ya ushindi inayojengwa juu ya kile Mungu amesema.”

OMBA NAMI;
Baba wa mbinguni, nakushukuru kwa nguvu ulizoziweka katika ulimi wangu. Nisaidie kila siku niwe na ukiri unao lingana na Neno lako, siyo hofu wala mashaka. Ninakiri ushindi, afya, amani, na baraka katika jina la Yesu. Amina.

Share

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles
Nguvu ya Neno la Mungu
Devotionals & EncouragementSwahili Articles

Nguvu ya Neno la Mungu

Andiko:“Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu kwa hekima yote…”...

Uwepo wa Mungu
Devotionals & EncouragementSwahili Articles

Uwepo wa Mungu

Katika safari yao kuelekea Kanaani, Musa hakutamani tu kufika kwenye nchi ya...

Kutoa kwa Imani na Moyo wa Furaha
Devotionals & EncouragementFinance & Stewardship in God’s WaySwahili Articles

Kutoa kwa Imani na Moyo wa Furaha

Mungu hathamini tu kile tunachotoa, bali moyo na imani iliyopo nyuma ya...

Ufalme Wake Kwanza
Devotionals & EncouragementSwahili Articles

Ufalme Wake Kwanza

Mathayo 6:33 (SUV): Bali utafuteni kwanza ufalme wa Mungu, na haki yake;...