Home Biblical Manhood - Men of Faith & Responsibility Baiolojia ya Wanaume Inavyochangia Kuwaua
Biblical Manhood - Men of Faith & ResponsibilityHealth & Christian BodySwahili Articles

Baiolojia ya Wanaume Inavyochangia Kuwaua

Share
Share

Takwimu kutoka Shirika la Afya Duniani la umoja wa mataifa WHO za mwaka 2021 zinaeleza kiwango cha wanaume kujiua ni mara mbili zaidi ya kiwango cha wanawake. Hii Inamaanisha katika wanaume 100,000 kuna uwezekano wa wanaume 12 kujiua. Kwa wanawake 100,000 kuna uwezekano wa wanawake 6  kujiua.

Takwimu hizi zimeshitua watu wengi na kuwasukumua wataalamu wa masuala mbalimbali ya ujinsia kufanya tafiti nyingi kutaka kujua sababu ni nini? Kwa nini wanaume? Yaani watu wa jinsia ya kiume, ambao huwa wanatarajiwa na kila mtu kuonyesha ushujaa, ushupavu, ubora kwenye utendaji wa mambo, uimara kwenye hisia zao na kila aina ya uhodari eti ndio wanaongoza kujiua kuliko wanawake!

Wataalamu wa afya hawakubaki nyuma katika tafiti hizi. Wao waligundua ugunduzi wa kushangaza sana. Kwamba kinachochangia wanaume kuongoza kujiua ni baiolojia yao wenyewe.  Kwamba kuna homoni ambayo inazalishwa kwa wingi kwa wanaume, ambayo ni Testosteroni. Homoni hii inapokuwa kwa kiwango ambacho hakijakusudiwa ndipo matatizo huja na kupelekea wanaume kupata hisia za kujiua.

Kivipi? Embu fuatilia wataalamu wanachofafanua:

Testosteroni  ni homoni inayopatikana kwa wingi kwa mwanaume inayozalishwa kwenye tezi dume inayofanya kazi ya kuchochea tabia mbalimbali za kiume kama vile ujasiri, na kupunguza hisia za hofu. Hii inapelekea wanaume kuwa na tabia ya ukimya kutokana na wasiwasi uliopunguzwa na homoni kwa kuchochewa ujasiri.

Homoni hii inakuwa imeongezeka kwa kiwango chake cha juu zaidi kwa mwanaume mwenye umri wa kati ya miaka  25 hadi 30. Ndio maana wanaume wengi katika umri huu wanaonyesha tabia za ujasiri kupita kiasi, ugomvi wa kupigana, kujitoa mhanga, na kuwa na hamu ya kufanya ngono.

Kiwango cha homoni kinashuka mwanaume akianza kufikia miaka ya 31 na kuendelea kwa kiwango cha asilimia 1% kila mwaka. Kuongezeka uzito wa mwili, uvutaji wa sigara na magonjwa ya zinaa yanaweza kuharakisha kushuka kwa testosterone.

Kushuka kwa Homoni ya testosteroni kunapelekea msongo wa mawazo, kudhoofu mwili, kupungua kwa mwitikio wa hamasa na kuongezeka kwa hatari ya kupata magonjwa ya kisukari.

Homoni ya Testosteroni inahusika katika kuongoza utendaji wa kemikali zinazohusika kusafirisha taarifa kutoka kwenye ubongo hadi kwenye misuli kwa ajili ya mwitikio. Hizi kemikali zinaitwa “neurotransmitters.”

Kushuka kwa Homoni ya testosterone kuna athiri pia utendaji wa hizi “neurotransmitters.”

Kwa kuwa wanaume ndio wenye testosterone ambayo inaongoza utendaji wa hizi kemikali, basi moja kwa moja athari zake zinamuathiri mwanaume zaidi kuliko mwanamke na kufanya uanaume kuwa teso.

Changamoto Katika Utendaji wa “Neurotransmitters”.

Hizi ni kemikali zenye kazi ya kusafirisha ujumbe kutoka kwenye ubongo kwenda sehemu mbalimbali kwenye mwili ili ogani za mwili zilete mwitikio unaohitajika. Zipo za aina tatu kulingana na kazi zake mahsusi: Dopamine, Serotonin na Norepinephrine.

Dopamine zina kazi ya kuchochea motisha, hisia za burudani (pleasure), hisia za ushindi na hali ya kufurahia maisha.

Zinapokosa udhibiti mzuri kutokana na kushuka kwa testosterone zinasababisha mwanaume akose hamasa na kupunguza hisia ya kuwa na msukumo, mwanaume anakosa uwezo wa kufurahia burudani kiasi ambacho yale mambo ambayo yalikuwa yanamburudisha na kumfurahisha hayafurahii tena wala hasikii kuburudika kuyafanya.

Hii ndio sababu kwa nini baadhi ya wanaume wanakosa hamu hata katika tendo la ndoa na jamii kuwahisi vibaya na kudhani wana uhanithi au waoga au wanachepuka kwa wale walio kwenye ndoa kumbe wana shida ya kibaiolojia na inapaswa kuangaliwa kitabibu.

Serotonin zina kazi ya kupunguza hali ya hasira na kuzuia hali ya kufanya maamuzi ya haraka yanayosukumwa na hasira.

Zinapokosa udhibiti mzuri au kuzaishwa kwa uchache zinapelekea mwanaume kuwa na hali ya hasira kiasi cha kufanya maamuzi ya haraka yanayosukumwa na hasira na matokeo yake maamuzi hayo yanaweza kuwa ya kufanya fujo, kutekeleza uhalifu, kuwaumiza wengine hata kujiua.

Hii ndio sababu kwa nini wanaume wanaongoza kushitakiwa kwa makosa ya jinai hasa yale yanayohusu ukatili na ugomvi. Jamii inawahukumu wanaume wa namna hii kwamba wasio na maadili wasijue kuwa wana changamoto kibaiolojia ambayo inaweza kutazamwa kitabibu pia na sio kutazamwa kimaadili tu.

Norepinephrine zina kazi ya kudhibiti mshtuko, nguvu, hali ya utayari na mwitikio wa msongo wa mawazo.

Zinapokosa udhibiti mzuri zinasababisha mwanaume kupooza,  kupata shida kumakinika (focus), kukosa hamasa na mazingira yanayomzunguka na mwitikio wa kihisia za kusizi au kufa ganzi.

Changamoto hizi kwa wanaume hazionekani dhahiri kwa nje kama ilivyo kwa wanawake. Kwa wanawake hisia za huzuni, kulia mchozi na hali ya kuhitaji msaada huonekana bila kificho na hivyo kuwa rahisi kushughulikiwa kitabibu.

Kwa upande mwingine, kwa wanaume kunakuwa na dalili za hasira kali ambayo huchukuliwa kawaida ya wanaume, hali ya kujitoa kafara kwa kufanya mambo yanayohatarisha maisha, kitu ambacho pia kinaonekana ni halali kwa wanaume kufanya, uraibu wa kutumia vitu na madawa pamoja na maumivu ya kimwili zaidi kuliko kihisia.

Dalili hizi huwa hazizingatiwi na watu zinapoonekana kwa mwanaume kwa sababu jamii inaamini ndivyo wanaume walivyo. Na wakati mwingine zinacukuliwa kama jambo la ki-haiba na kimaadili zaisi kuliko kuchukuliwa kama jambo la kibaiolojia linalotakiwa kutibiwa kitabibu.

Njia za Kuzuia

1. Kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi na kuzingatia lishe bora.

Mazoezi na lishe bora ni njia mojawapo ambayo imethibitishwa kitaalamu kudhibiti kupungua na kuongezeka kwa homoni ye testosteroni. Mazoezi ya mwili kwa wastani husainia himoni hii kuwa katika kiwango chake cha wastani kinachotakiwa na kwa hivyo kuzuia madhara yatokanayo na kushuka kwa kiwango cha homoni ya testosteroni.

Lishe bora pia inapoendana na mazoezi kuzuia mwili kutunza kiwango kikubwa cha sukari ambacho hakihitajiki kinachoweza kusababisha mrundikano wa mafuta na kuongeza uzito wa mwili.

Wanaume wengi wanateswa na magonjwa ya moyo kwa kukosa utamaduni wa mazoezi na kuwa na lishe mbovu inayofanya mafuta kurundikana kwenye mishipa na maeneo yazungukayo moyo.

Vile vile kuna wanaume ambao wanasumbuka na tatizo la uume kuwa mdogo na kukosa uwezo wa misuli yake kukaza inavyotakiwa na kuwafanya kuwa na hofu ya kudharauliwa na wenza wao.  Hii inatokana na unene ambapo mafuta hurundikana kwenye maeneo ya shina la uume na kufanya shina la uume limezwe na mafuta na uume kuonekana mdogo. Kwa kuzingatia lishe bora, tatizo hili linaweza kuepukwa.

2. Kuzungumza kwa uwazi changamoto zako

Si ajabu kwa mwanaume kuumizwa, si jambo la ajabu kwa mwanaume kuzungumza hisia zake, si jambo la ajabu kwa mwanaume kulia. Tafuta mtu au watu wa kuzungumza nao kuhusu unachopitia wazi wazi ili kupata msaada wa haraka na kutua mzigo mzito moyoni.

Jitahidi sana kuwa na watu wa karibu ambao unaweza kuzungumza nao mambo yako mara kwa mara. Usife na tai yako shingoni.

Nimeandika kitabu ambacho kitawasaidia wanaume kujua mzizi wa mateso na mahangaiko yao ya siku zote, njia za Kuondoa hivyo visababishi na kuishi maisha marefu yenye furaha bila majuto. Kinaitwa UANAUME WAKO USIWE TESO LAKO. Kama unahitaji nakala yako, wasiliana na mwandishi kwa namba za simu 0657342567.

Share

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *